ACHOMA NYUMBA YAKE KUPOZA HASIRA
MAZITO MUME ACHOMA NYUMBA KUPOZA HASIRA! MWANAUME mmoja aliyefamika kwa jina la ‘Mlawa’ mkazi wa Kizani, Gezaulole jijini Dar amedaiwa kuchoma nyumba yake na kupoza hasira alizokuwa nazo. Kwa mujibu wa mashuhuda, jamaa huyo anadaiwa kufanya tukio hilo kutokana na kuwa na ugomvi na mkewe Zubeda Maarufu aliyezaa naye watoto watatu. “Alikuwa na ugomvi na mkewe, aliondoka hapa na kwenda kuishi na mwanamke mwingine sasa ndio hivi juzi tukashangaa amekuja kuchoma nyumba,” alidai shuhuda aliyeomba hifadhi ya jina. mke huyo wa Mlawa, alisema kuwa siku ya tukio yeye na wanawe walikuwa wamehamia kwa jirani yao baada ya mumewe huyo kufanya jaribio la awali la kuchoma moto kisha kushindwa. “Kabla ya tukio hilo alikuja siku ya Jumatano akamwaga petroli huku akidai kuwa anawasha nyumba moto lakini bahati nzuri tuliwahi kumuona na majirani wakanisaidia akaondoka,” alisema mke huyo wa Mlawa na kuongeza:“Siku ya Ijumaa ndipo alipokuja tena mida ya saa tatu usiku mimi nikiwa kwa jirani yangu maan...