Maajabu ya Simba
BWANA SIMBA, THE KING OF JUNGLE!
Simba kwa kiingereza anafahamika kama lion na jina
lake la kisayansi (scientific name) anafahamika kama panthera
leo na koo(Genus) yake ni panthera, hii koo panthera
inajumuisha na wanyama wengine ikiwemo tiger wa bara la
asia, chui, American jaguar, na mnyama anaefahamika kama
puma au mountain lion.
Simba yupo kwenye order ya wanyama walaji wa nyama
almaarufu carnivore na familly yake inaitwa felidae, hii familly
ya felidae inajumuisha paka wote wanaopatikana duniani
ikiwemo wanaofugwa manyumbani, paka pori, simba, chui,
tiger, jaguar na wengineo jamii ya paka ikiwemo cheetah
(Duma).
Simba ndiye paka mkubwa Africa na anashika namba mbili
duniani baada ya tiger ambaye anapatikana barani Asia pekee
dunia nzima na simba pekee ambaye huishi katika makundi
miongoni mwa wanyama jamii ya paka na kundi lao linaitwa
(pride) pia simba ni wanyama wanaopendelea kuishi maeneo
wazi yenye nyasi(Open area) kama ngorongoro crater na
Serengeti national park.
Simba pia anafikia hadi uzito wa kg 220-250 kwa dume na
upande wa jike ni kg 100-120 na katika familia ya simba ni
majikee pekee wanaofanya shughuli ya uwindaji (hunting ) na
madume wao hubaki na watoto na majike wakishaua mnyama
simba dume ndo huanza kula kisha watoto na baadaye jike
ilihali wao ndo wawindaji.
Pia simba ndo wanyama wanaoongoza kwenda fungate
(Honeymoon ) na huenda kwa takribani wiki mbili, iko hv kwa
kuwa hawa wanaishi katika makundi dume na majike ikitokea
katika ile familia kama kuna jike ambaye yuko heat hua
anamchukua dume wanaenda mbali kidogo na ile familia kwa
ajili ya kufanya mating kwa huo muda wa wiki mbili na kabla
ya kwenda fungate kwa kawaida yule jike anayehitaji kwenda
fungate na dume huwa anamuwindia dume chakula kizuri
chenye mafuta ambacho kitamshibisha yule dume na wakiwa
fungate huwa hawali kitu chochote wanakunywa maji tu kwa
huo mda wa wiki mbili na huwa wanajamiana kila baada ya
dakika saba (sasa ebu fikiria siku ina dakika saba ngapi na
kwa huo mda wa wiki mbili dume atampanda jike mara ngapi).
Simba pia hupendelea kuwinda wanyama kama mbogo,
pundamlia, nyumbu na baadhi ya swala na kwa kawaida simba
dume ana uwezo wa kula hadi Kilo 15 za nyama na akishakula
hizo kilo 15 huwa anauwezo wa kukaa siku tatu mpaka wiki
moja bila kula halafu ndo anakuja kuwinda tena.
Katika kuwinda kwao wanatumia staili kuu tatu ya kwanza ni
sporting ( wanaangalia mnyama wa kumuwinda), ya pili ni
stalking ( wananyemelea ) na ya mwisho ni ambush ( kuvamia)
na wakishakamata mnyama huwa wanakimbilia kuuma
shingoni ili kumbana pumzi(suffocate) na sio kunyonya damu
kama wengi wanavyodhani na kwa kawaida simba jike hubeba
ukauzito kwa mda wa miezi 3 na anazaa kuanzia watoto 2-4.
Sasa unaweza ukajiuliza kama jike la simba hubeba ujauzito
kwa huo mda na kujifungua watoto wengi mbona simba ni
wachache? Iko hv hawa wanaishi kwenye makundi dume
akimiliki majike wake na huwa hawa madume wenye familia
wanachallengiwa na madume ambao hawana familly kwa ajili
ya kimiliki zile familly na ikumbukwe sio madume wote wa
simba wanamiliki familia sasa ikitokea kwa bahati mbaya huyu
simba mwenye family akapigwa na dume mwenzake ambaye
hana family huyu dume ambaye hana family atachukua ile
family ya yule dume aliyempiga na kuitawala yeye na kwenye
ile family akikuta kuna watoto wa yule dume aliyempiga
atakachofanya huyu dume atawaua wale watoto wote kwa
sababu hawezikulea damu isiyoyake na anafanya vile ili jike
mwenye wale watoto apatwe na uchungu aingie kwenye heat
ili ambebeshe mimba yake na kama kwenye ile familia kuna
jike mwenye ujauzito atakachofanya huyu dume atamchukua
yule jike atamtoa nje ya family na ataforce kumpanda hadi ile
mimba itoke then anampachika mimba yake.
Vile vile hawa simba dunia nzima wanapatikana Africa na Asia
na katika bara la asia wanapatikana pale india pekee katika
msitu unaoitwa geyforest. Vilevile hawa simba ndo wanyama
wanaoongoza kulala kwa siku hulala masaa 16 na kufanya
kazi masaa 8 na kawaida wanawinda usiku na wakati
mwingine mchana pale hali inaporuhusu na hawa ni
wachangamfu mchana na usiku (diurnal and nocturnal ) yaani
wao huona usiku na mchana. Huyo ndo bwana simba (king of
jungle ) kama wengi wanavyopenda kumwita.

Maoni
Chapisha Maoni