Kilichonipata baada ya kumpenda bint ambae alikua mwalimu
Nilikutana na Binti mmoja ambae alikua mwalimu,tukapendana na kuahidiana kuoana.
Basi kwakua yeye alikua akifundisha kijijini na mimi nilikua naishi Dar es Salaam,niliamua kwanza kumuhamisha kutoka huko kijijini kumleta hapa mjini. Nilijibana na visenti vyangu nikaanza harakati za kumuhamisha.
Alipokea kwa furaha sana swala la yeye kuhamia hapa Dar es salaam.mipango ikakamilika akaja Dar es salaam na kuanza majukumu yake ya kujenga taifa la baadae ( Kufundisha) ajabu ni kwamba binti huyu mwalimu pamoja na elimu yake lakini elimu haikumuinua ila vilikua vyeti tu vya kumpatia kipato lakini sio kumpa maarifa ya maisha.Alibadilika ghafla na kulimbuka na jiji kwa kuparamia vijana waliomrubuni kwa tamaa.
Pamoja ya kua nilimpangia nyumba lakini siku moja nikitoka safari hasa ukizingatia kazi zangu ilikua ni kusafiri nje ya Dar es salaam,siku moja niliporudi nilikwenda anapoishi na kumkuta akiwa sebuleni amelewa chakari na kijana mmoja ,mbaya zaidi walifanyia hapo huo uchafu wao na kutupa kondomu zilizotumika zikitapakaa sebuleni,nilipofungua mlango na kuona kwa macho yangu maajabu hayo nilichukua nguo zangu na kuondoka zangu nikiwaacha waendelee na maisha waliyoyachagua wao wenyewe.
Mbaya zaidi yule kijana alimshawishi achukue mkopo ili wafanyie biashara na alipochukua huo mkopo kijana aliingia mitini na pesa zote na sasa bint anahangaika pekeake kulipa deni asilonufaika nalo.
Wazazi wengi wanmasomesha watoto wao kwa shida sana wengine huuza mali zao,mashamba hata viwanja na nyumba ili mtoto wake asome aje amsaidie lakini binti akishapata kazi anamuawaza hawara na kuona bwana ndio kili kitu akiwaacha wazazi wake wakiteseka ilhali umri umeshaenda,
picha haihusiani na tukio:
Rafiki yangu Hassan Mwagilloh nilipompa kisa hiki aliniambia mabinti wengi walio kwenye taaluma ya elimu hawajatulia japo wapo wanaojielewa,
anasema hata yeye mwaka 2006 alimposa binti ambae wakati huo hakua mwalimu ila alishamaliza kidato cha sita ,mwaka 2007 serikali ilitangaza dharura ya kuwaajiri wanafunzi waliomalia kidato cha sita na kupata alama nzuri ili kutatua tatizo la upungufu wa walimu uliokuwepo wakati huo.
Ilikua wanapewa kozi ya mwezi mmoja kisha moja kwa moja wanaajiriwa hivyo nae akampa dili hilo huyo mchumbaake au mkewe mtarajiwa.
Ajabu huyu binti alipoaanza kazi huko kusini akaanza mabadiliko mara hapatikani nk. kumbe huko huko kazini akapata bwana aliemchanganya huko kijijini,penzi lilikua moto moto mpaka binti akapata ujzuzito na kipindi chote hicho akawa hapatikani mana line aliyonunuliwa na huyu jamaa yangu akaigawa kwa mtu na akipigiwa huyo mtu hatoi maelezo yoyoe.Baada ya mwalimu kupata ujauzito yule kijana akamuona rafiki wa yule mwalimu yaanrafikie ndio akaoleewa na yeye akatelekezwa na mimba halafu mbaya zaidi wote wanafanya kazi shule moja haikwepeki ukiamka asubuhi unawaona,mwalimu aliumia mno ikapelekea kuacha kazi na kwenda kusoma Udom na mpaka sasa hajaolewa na hana kazi ,haya ni mambo ya kujifunza kwa hawa binti zetu,dada zetu na mama zetu muwe makini kipindi cha ujana kwani mtu wa maana mnaweza kumkataa kwa muonekano wake na mazingira kisha ukamtaka muharibifu asiejua thamani yako,kuna tofauti ndogo sana kipindi cha ujana wa msichana na uzee wake usipotulia na kufanya maamuzi sahihi utaishia kulia maisha yako yote.

Maoni
Chapisha Maoni